Numbers 33

Vituo Katika Safari Ya Waisraeli

1 aHivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni. 2 bKwa agizo la Bwana, Musa aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:

3 cWaisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 4 dwaliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
5 eWaisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
6 fWakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
7 gWakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8 hWakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
9 iWakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
10 jWakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
11 kWakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
12Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
13Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
14 lWakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.
15 mWakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
16 nWakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.
17 oWakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.
18 pWakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.
19Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.
20 qWakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.
21Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.
22Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.
23Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.
24Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.
25Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.
26Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.
27Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.
28Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.
29Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.
30 rWakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.
31 sWakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.
32 tWakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.
33 uWakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.
34Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.
35 vWakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.
36 wWakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
37 xWakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 38 yKwa amri ya Bwana, kuhani Haruni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. 39Haruni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.
40 zMfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.
41Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.
42Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.
43 aaWakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.
44 abWakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.
45 acWakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.
46 adWakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.
47 aeWakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.
48 afWakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.
49 agHuko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.

50 ahKatika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Musa, 51 ai“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, 52 ajwafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada. 53 akMtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. 54 alMtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.

55 am“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. 56 anKisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”
Copyright information for SwhKC